KOCHA MWADUI FC ANASA SIRI ZA YANGA

KOCHA Mkuu wa timu ya Mwadui FC, Ally Bizimungu, amesema amebaini jeuri ya kikosi cha Yanga ilipo, lakini wamejipanga kupambana nao ili waweze kuibuka na pointi tatu ugenini kesho.

Bingwa - - HABARI -

Kikosi cha Mwadui kilichofungwa na Yanga mabao 2-0 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa katika dimba la Kambarage, Shinyanga, kitamenyana na Wanajangwani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA jana, Bizimungu alisema amewasoma Yanga kwa muda mrefu katika mechi walizocheza na kubaini ubora na udhaifu wao, hivyo amefanyia kazi mapungufu yao kabla ya kuwakabili kwa mara nyingine.

Alifafanua kwamba kikosi cha Mwadui kilichokutana na Yanga katika mzunguko wa awali ni tofauti na kilivyo sasa, kwani walifanya usajili mzuri kipindi cha dirisha dogo.

“Tumejiandaa vizuri kukabiliana na Yanga baada ya kugundua nguvu yao ilipo na mapungufu na kufanyia kazi mambo muhimu, hivyo hatuna wasiwasi wowote,” alisema Bizimungu.

Aidha, aliongeza kuwa katika mchezo huo atawakosa wachezaji wawili, Mathias Gerald anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano na Iddy Mobb ambaye ni majeruhi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.