BEATRICE AFANYA KWELI TENISI A/AFRIKA MASHARIKI

Bingwa - - HABARI - NA GLORY MLAY

BEATRICE Kimaro, mchezaji wa tenisi kutoka Tanzania, amemshinda Tracy Gaga wa Rwanda seti 2-0 katika raundi ya pili ya fainali ya michuano ya Afrika Mashariki na Kati, chini ya umri wa miaka 16, inayoendelea kwenye Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam.

Beatrice alishinda 6-2, 6-1, wakati Esther Nankulange alimchapa Irakoze Belyse kwa seti 2-0 za 6-1, 6-1.

Katika mchezo wa wachezaji wawili ‘doubles’, Irakoze Belyse na Tracy Gaga walifungwa na Esther Nankulange na Victoria Ndossi kwa seti 2-0 za 6-3, 6-1.

Naye Moses James wa Tanzania alifungwa na Kashid Moussa wa Burundi kwa seti 2-0 (6-1, 6-1), huku Rashidi Ramadhani pia wa Tanzania akimshinda Abdoul Nduwimana wa Burundi 6-4, 6-3.

Kwa upande wa wanaume wachezaji wawili wawili, Kashid Moussa na Abdul Nuru walishinda kwa seti 2-0 za 6-2, 6-1 dhidi ya Mella Nicholas na Rashid Ramadhan wa Tanzania.

Katika mchezo uliofuata, Godfrey John wa Tanzania alifungwa seti 2-0 (6-1, 6-0) na Kael Shah wa Kenya, huku Kanuti Alawa wa Tanzania naye pia akifungwa kwa seti 2-0 (6-2, 6-2) na Derrick Ominde wa Kenya.

Mchezo mwingine ulikuwa kati ya Joseph Mfashingabo wa Rwanda ambaye alimfunga Rouched Hassan wa Comoro kwa seti 2-0 za 6-1, 6-0.

Raymond Odour wa Kenya alimshinda Traves Gideon wa Shelisheli kwa seti 2-0 (6-1, 6-0), huku Emmanuel Mwanishimwe wa Rwanda akimshinda Gureb Jafar wa Somalia kwa seti 2-0 za 6-1, 6-0.

Mchezaji wa timu ya Uzuri Star, Shabebe Yusuph (kushoto), akiwania mpira na mchezaji wa Morning Star, Hamis Kilama, katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Kinesi, Dar es Salaam jana. PICHA: IMANI NATHANIEL.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.