Sarri alilia mrithi wa Fabregas

KOCHA Maurizio Sarri ameitaka Chelsea kusajili nyota atakayemsaidia Jorginho, baada ya staa wao, Cesc Fabregas, kuondoka mwishoni mwa wiki na kwenda kujiunga na klabu ya AS Monaco ya Ufaransa.

Bingwa - - MAKALA -

Juzi Chelsea walifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Newcastle United, wakiwa katika dimba lao la Stamford Bridge na huku Jorginho siku hiyo ikionekana kuwa mbaya kwake.

Katika mchezo huo, nyota huyo wa timu ya Taifa ya Italia alipoteza mipira mingi na akishindwa kuitafuta na huku akitoa pasi ambazo hazikuwa na mwelekeo.

Kufuatia hali hiyo, mashabiki wengi wa Chelsea walionekana kumlalamikia na Sarri anakubali kuwa nyota huyo wa zamani wa Napoli yupo katika kipindi kigumu, lakini anasema alishindwa kumpumzisha kwani hakuwa na mchezaji mwingine kwenye benchi.

"Jorginho alikuwa katika wakati mgumu na kwenye benchi sikuwa na mchezaji wa kumbadilisha," alisema Sarri. "Nahitaji walimsaidia Jorginho. Ila sifahamu ni ni lini atawasili na klabu ina wasiwasi na inafahamu mawazo yangu,” aliongeza kocha huyo.

Chelsea ilipata ushindi huo kwa mabao yaliyofungwa na mastaa wao, Pedro na Willian wakati la wapinzani lilifungwa kwa kichwa na Ciaran Clark.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.