Bingwa - - MAKALA -

Kauli ya kocha huyo imekuja baada ya wiki iliyopita jarida la El Mundo kudai kuwa Neymar Sr, aliupigia uongozi wa Barca akiutaka umrejeshe mwanawe huyo Camp Nou, ambaye alijiunga na klabu ya Paris Saint-Germain mwaka juzi kwa ada ya Euro milioni 222.

Hata hivyo, Neymar Sr naye ameshakanusha taarifa hizo na sasa Valverde anasema kwamba, kama kuna simu yoyote iliyowahi kupigwa haikuhusiana na jambo hilo.

"Watu wamekuwa wakipenda kuzungumza mambo makubwa kuhusu wachezaji ambao wapo kwenye klabu nyingine," kocha huyo aliwaambia waandishi wa habari.

"Ni mchezaji mkubwa, lakini kwa sasa yupo kwenye klabu nyingine hivyo hakuna cha kuzungumza zaidi kuhusu jambo hilo,” aliongeza kocha huyo.

Alisema kwamba mara nyingi habari kama hizo zimekuwa zikijitokeza kwenye vyombo vya habari na mchezaji huyo ni wa PSG na akasema kwamba, wanaiheshimu klabu hiyo. ushindi huo wa bao 1-0 na kuwafanya kuwa mbele tena kwa pointi saba dhidi ya Tottenham na Man City ambazo siku hiyo hazikucheza.

"Ilikuwa ni mechi ngumu sana na hivyo ndivyo tulivyotarajia. Ulikuwa ni mchezo mgumu, mgumu mno,” alisema Klopp. "Kila mtu anajua ni vigumu kwenda Brighton. Utatakiwa kuwa na ubunifu dhidi ya timu ambayo imejipanga na inayofanya mashambulizi ya kushtukiza na inayocheza mipira mirefu kwa asilimia 50,” aliongeza kocha huyo.

"Ulikuwa ni utendaji mzima kabisa kutoka upande wangu. Msimu huu ambao kuna ujuzi mpya na tunapaswa kuwa katika hali kama hiyo ya ukomavu,” aliongeza zaidi Klopp. LONDON, England

KAMA umesahau kitendo cha Arsenal kumsajili Pierre-Emerick Aubameyang kwa kitita cha pauni milioni 60 mwaka jana, ndicho kilichopunguza mawazo na huzuni na kuamsha mwanga wa matumaini miongoni mwa mashabiki wengi wa klabu hiyo.

Arsenal ilifanikiwa kumnasa mpachika mabao huyo katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili wa mwezi kama huu, kazi kubwa ikifanywa na Arsene Wenger. Kocha huyo wa zamani wa Arsenal, alijikuta kwenye wakati mgumu kusaka mfungaji mzuri wa mabao hasa baada ya kuondokewa na nyota watatu; Olivier Giroud, Theo Walcott na Alexis Sanchez. Baada ya kufanikiwa kumpata Aubameyang, nyota huyo amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuibeba timu hiyo, licha ya kwamba kwa namna moja au nyingine umuhimu wake hauzungumzwi sana.

Tangu afunge bao lake la kwanza katika mechi ya kwanza kuitumikia Arsenal, mnamo dakika ya 37 ya mchezo wao dhidi ya Everton, Aubameyang ameshafunga jumla ya mabao 24 kwenye mechi 34 za Ligi Kuu England.

Kwenye takwimu hiyo, Mgabon huyo amepitwa na nyota wa Liverpool, Mohamed Salah tu ambaye amefunga mabao 27.

Zaidi ya hapo, kwenye zile ligi tano kubwa za Ulaya, wachezaji pekee waliomzidi Aubameyang kwa jumla ya mabao ni Cristiano Ronaldo (32) na Lionel Messi (30).

Umuhimu huo mkubwa wa Aubameyang umekuja katika nyakati ambazo Arsenal ina uhaba wa wachezaji wabunifu ambao kazi yao ya kutengeneza nafasi za mabao ingemalizwa vizuri na straika huyo.

Ikumbukwe miaka iliyopita, mashabiki wa Arsenal walikuwa wanalilia klabu yao isajili mpachika mabao hodari wa kumalizia kazi za akina Cesc Fabregas, Samir Nasri na Andrey Arshavin, lakini kwa sasa wote hawapo. Mchezaji pekee wa Arsenal mwenye uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi za mabao ni Mesut Ozil ambaye hata hivyo, ameana mechi mbili tu za Ligi tangu katikati mwa Novemba mwaka jana. Mwingine ni Aaron Ramsey ambaye amebakiza miezi michache kabla ya kuondoka Arsenal kujiunga ra Juventus ya Italia, hivyo kuacha majukumu kwa Alex Iwo Lakini cha ajabu, mpaka sasa Iwobi hajaweza kutoa pasi ya bao hata

moja ambalo

limefungwa na Aubameyang kwenye Ligi Kuu England.

Pia, unaweza ukashangaa kusikia hili, lakini takwimu zinaeleza kwamba Aubameyang alipokuwa Dortmund aliweza kutoa pasi 20 za mabao katika mechi 134 za Bundesliga na tangu atue Arsenal, jukumu hilo limehamia kwake.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.