Koulibaly, piga ua lazima atue Manchester United...Uk

Bingwa - - JUMATATU SPESHO -

ambako kulikuwa na Nicolas Gyan na Mohamed Hussein. Mara nyingi timu zinazomiliki na kushambulia mara kwa mara hushambuliwa au kufungwa kwa mabao ya kushtukiza, baada ya timu pinzani kupora mpira na kupiga pasi ndefu kwa mchezaji aliyekuwa mbele. Hilo halikufanikiwa kwa JS Saoura lakini ubora wa wachezaji wao upo miguuni mwao kwani wana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na kuwalazimisha wapinzani kufanya makosa. Katika michezo yao waliyotumia kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, walifunga mabao manne huku matatu yakipatikana kwa mikwaju ya penalti. Maana yake kuwa wana uwezo mkubwa wa kuifanya timu pinzani kufanya makosa kama kucheza rafu ndani ya eneo lao la mwisho. Kutokana na hilo, Aussems alijaza viungo ambao walifanikiwa kuwasukuma wapinzani hasa viungo wa JS Saoura kucheza mbali na eneo la mwisho la Simba huku mbele akibaki mchezaji mmoja pekee ambaye hakuwa na madhara kwa mabeki wa Simba. Mkude na Kotei kwa pamoja waliisaidia timu kwenye ulinzi huku Chama na Dilunga walikuwa na kazi ya kuisukuma timu kwenda mbele wakihakikisha wanapeleka mipira kwa washambuliaji wao. Moja ya maeneo ambayo yanaonyesha udhaifu mkubwa kwenye kikosi cha Simba, basi ni safu yao ya ushambuliaji.

Licha ya kufunga mabao matatu bado akina Okwi, Kagere na John Bocco hushindwa kutumia vizuri nafasi ambazo zinatengenezwa.

Hiyo si mara ya kwanza katika michezo mingi waliyoshinda au kufungwa wamekuwa wakifanya hivyo kiasi cha kuamini wanakosa umakini pindi wanapokuwa kwenye eneo hilo la mwisho la mpinzani.

Lakini uwezo binafsi wa washambuliaji wao umekuwa ukizaa matunda kwa kikosi hicho, tazama jinsi Okwi alivyofunga bao la kwanza kwa ustadi mkubwa kisha kutoa pasi mbili kwa Kagere.

Ili uweze kufanikiwa zaidi kwenye michezo ya makundi lazima uwe na wastani mzuri wa kufunga mabao ikiwa tayari Simba wamefunga matatu huku wakikosa nafasi zaidi ya tatu.

Wakati mwingine mabao yanatoa nafasi kwa timu husika kusonga mbele au kubaki huku kukiwa na mifano mingi tu ambayo imewahi kutokea.

USHAMBULIAJI NUSU KWA NUSU MCHEZO UJAO

Mchezo unaofuata Simba watasafari kuwafuata AS Vita ambao walifungwa mabao 2-0 na Al Ahly juzi usiku.

Mchezo ambao wenyeji hao watautazama kwa jicho la tatu zaidi ikiwezekana kushinda ili kupata pointi tatu katika uwanja wao wa nyumbani.

Kwa maana hiyo, Simba wanatakiwa kujipanga kweli sababu wapinzani wao wana wachezaji wenye uwezo mkubwa ikumbukwe msimu uliopita walicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kufungwa dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco.

AS Vita wanacheza soka la pasi fupi fupi lakini mara nyingi hubadilika kutokana na mpinzani wanayekutana naye, wachezaji wao wana uwezo mkubwa wa kukaa na mpira na kuleta madhara.

Simba wanatakiwa kulifanyia kazi eneo lao la ulinzi na kuongeza umakini kwenye ushambuliaji kwani kwa aina ya mchezo huo lazima uhakika wa kufunga bao uwepo kwa kila nafasi itakayotengenezwa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.