GWIJI LEEDS UTD, AFRIKA KUSINI AFARIKI DUNIA

Bingwa - - TANGAZO -

KLABU ya Leeds United na timu ya taifa ya Afrika Kusini, zimepata pigo baada ya kuondokewa na straika wao wa zamani, Phil Masinga, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 49.

Taarifa za kifo cha Masinga ambacho kilitokea jana asubuhi, zilithibitishwa na Rais wa Chama cha Soka Afrika Kusini, Danny Jordan, ambaye alisema nyota huyo alifariki baada ya kuumwa kwa muda mrefu.

Masinga aliitumikia Leeds kwa misimu miwili, kati ya mwaka 1994 na 1996, pia aliwahi kuzichezea timu za Bari na St. Gallen ingawa alifanikiwa zaidi alipokuwa Mamelodi Sundowns kabla ya kuhamia England.

Masinga alitinga uzi wa Afrika Kusini katika mechi 58 na aliweza kufunga bao lililoiwezesha timu yake hiyo kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia 1998 kwa mara yao ya kwanza.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.