Mbelgiji amaliza kazi kwa Mbabane Swallows

Dimba - - News - NA SAADA SALIM

BAADA ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutangaza mpinzani wa Simba, Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Patrick Aussems, ameibuka na kuwatoa hofu mashabiki wa timu hiyo na kuwataka wakae mkao wa kula, kwani vijana wao anawaaminia.

Simba wamepangwa kucheza na Mbabane Swallows ya Swaziland, ambapo wekundu hao wa Msimbazi wataanzia kukipiga nyumbani mchezo unaotarajiwa kuchezwa kati ya Novemba 27 na 28, huku marudiano yakipangwa kati ya Desemba 4-5 ugenini.

Wekundu hao wa Msimbazi wanaendelea kujifua jijini Dar es Salaam, huku nyota wake 12 wakiwa na vikosi vyao vya timu za taifa wakizitumia kwa ajili ya michuano ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika.

Akizungumza na DIMBA, Aussems alisema ameona ratiba na atatumia kila njia kuwasoma vizuri wapinzani wao ili watakapokutana iwe rahisi kwao kuwaadhibu.

Kwa upande wa beki wa timu hiyo, Erasto Nyoni, aliyewahi kukutana na wapinzani hao msimu wa 2017 akiwa na timu yake ya zamani ya Azam, alisema wakati huu wapinzani wao hao hawatabakia salama.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.