Yanga kujipima kwa African Lyon

Dimba - - News - NA TIMA SIKILO

KIKOSI cha Yanga leo kinatarajia kushuka dimbani kumenyana na African Lyon katika mchezo wa kirafiki utakaochezwa kwenye Uwanja Uhuru, Dar es Salaam.

Yanga imepanga kutumia mchezo huo kuwapima wachezaji wake katika kipindi cha mapumziko ya Ligi Kuu Tanzania Bara kupisha michezo ya kimataifa ya kalenda ya Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA).

Wanajangwani hao kwa mara ya kwanza msimu huu watatoka kwenda kucheza nje ya Dar es Salaam, michezo miwili Kanda ya Ziwa dhidi ya timu za Mwadui FC Novemba 22, kabla ya kuivaa Kagera Sugar Novemba 25.

Akizungumza na DIMBA, Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh, alisema mchezo huo utakuwa kipimo kwa kikosi chao, kwani kitawasaidia kubaini mapungufu kabla ya timu hiyo kusaka pointi sita nje ya Dar es Salaam.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.