Njombe Junior bingwa Hellen Cup

Dimba - - News - NA GLORY MLAY

TIMU ya Njombe Junior imeibuka mabingwa wa Kombe la St. Hellen baada ya kuifunga Machuya FC mabao 2-0, katika mchezo uliopigwa juzi, mkoani humo. Mabao ya washindi yalifungwa na Josse Mlingo dakika za 23 na 78 na kufanya timu hiyo kuibuka na kitita cha Sh 300,000, huku mshindi wa pili akichukua Sh 100,000. Akizungumza na DIMBA, mratibu wa michuano hiyo, Shukuru Milinga, alisema kwa mwaka huu michuano hiyo imeshirikisha timu 16, zikitokea kata mbalimbali katika mkoa huo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.