NANDY

ATUMIA SIKU 366 KUIPIKA ËAFRICAN PRINCESSÍ

Dimba - - Burudani - MA JESSCA NANGAWE

MSANII Faustine Charles, maarufu kama Nandy, amesema ametumia mwaka mzima kuandaa albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la ëAfrican Princessí.

Akizungumza na DIMBA, Nandy amesema imemchukua mwaka mzima kuandaa albamu hiyo, ili kupata kitu kizuri na pia kitendo cha kusafiri kila wakati kimekuwa moja ya sababu za msingi za kuchelewa.

ìMashabiki walikuwa wakinitaka nitoe albamu, ingawa nina muda mfupi kwenye muziki, lakini niliwaahidi nitatoa kitu kizuri na ndilo lengo langu, huu ndio wakati mwafaka wa mashabiki kufaidika na mimi,î alisema Nandy.

Albamu hiyo ina nyimbo 13 na aliizindua rasmi siku ya Ijumaa katika ukumbi wa Next Door Arena, uliopo Masaki.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.