Diamond

ammwagia neema Hawa

Dimba - - Burudani - NA JESSCA NANGAWE

LICHA ya staa wa Bongo fleva Naseeb Abdul ëDiamondí kugharamia matibabu kwa msanii mwenzake Hawa Said, amedai bado ataendelea kumsaidia fedha za kuanzisha mradi wowote wa kujiingizia kipato.

Akizungumza na DIMBA, Diamond alisema amefarijika kuona matibabu ya msanii huyo yanakwenda vyema na kuahidi kutaka kumsaidia zaidi, huku akimtaka kumpa wazo la biashara anayotamani kufanya.

ìNafarijika kuona una tabasamu, sasa nitafurahi kusikia wazo zuri la biashara kutoka kwako ili nikuwezeshe,î alisema Diamond kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.

Msanii huyo aliwezeshwa fedha za Hawa kwenda kutibiwa nchini India ambako alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa mapafu kujaa maji.

Hawa, aliyeimba na Diamond wimbo wa ëNitarejeaí, anatarajia kurejea kutoka India wakati wowote baada ya afya yake kuimarika. Diamond alidaiwa kutumia zaidi ya Sh milioni 50 kusimamia matibabu yake.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.