Kumbe Davina naye ni Mama Lishe

Dimba - - Burudani - NA JESSCA NANGAWE

MSANII kutoka kiwanda cha Bongo Movie, Halima Yahaya, maarufu kama Davina, amesema kwa sasa hakuna staa anayeendekeza starehe zaidi ya kuchakarika na kazi za kujiingizia kipato.

Akizungumza na DIMBA, Davina amesema mastaa wengi, hasa wanawake wamekuwa makini katika kutafuta pesa, huku wakitumia muda mwingi kubuni miradi ya biashara.

ìNaona wengi kwa sasa wanajielewa na wanatambua nini maana ya maisha, ukiniuliza mimi mara ya mwisho kwenda saluni sijui ni lini, nipo busy nashinda jikoni nikiwaandalia wanafunzi wa UDSM chakula, sidhani kama kwa sasa yupo staa anayetumia muda wake tu na mambo ya starehe, wengi tunajielewa,î alisema Davina.

Davina amesema amekuwa akiwakubali sana Wolper na Shilole, kwani licha ya kuwa na majina makubwa, wamekuwa wakifanya biashara ambazo zinaonekana ni za watu wa chini na lakini zikiwaingizia pesa nyingi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.