Mtibwa Sugar mbele kwa mbele

Dimba - - Dimba - NA JESSCA NANGAWE

KIKOSI cha Mtibwa Sugar ya Turiani mkoani Morogoro, kimefanikiwa kusonga mbele hatua inayofuata ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Northen Dynamo ya visiwa vya Shelisheli.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Mtibwa Sugar walishinda mabao 4-0 na ushindi wa jana unawafanya kufunga jumla ya mabao 5-1.

Ushindi wa Mtibwa Sugar inakuwa ni furaha kwa Watanzania wote kwani Simba nao wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mbabane Swallows ya Eswatini na kuwafanya kufunga jumla ya mabao 8-1.

Bao pekee la Mtibwa lilifungwa na Haruna Chanongo na sasa Wakata Miwa hao watakutana na KCCA ya Uganda katika mchezo unaokuja ikiwa ni nafasi nyingine ya kujitangaza kimataifa.

Kwa upande wa timu za Zanzibar zimeonekana kuyaaga mashindano hayo mapema baada ya Zimamoto kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 kabla ya awali kukumbana na kipigo cha mabao 4-0 ikiwa ugenini dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

JKU nao wanakutana leo wakiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Amaan dhidi ya Al Hilal ya Misri katika mchezo wa marudiano baada ya awali kufungwa ugenini mabao 4-0.

USHINDI

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.