Beki KMC amchimba mkwara Chirwa

Dimba - - Dimba - NA TIMA SIKILO

BEKI kisiki wa timu ya KMC, Ali Ali, amesema anajifua vikali kuhakikisha anawadhibiti mastraika wa Azam FC wanaoongozwa na Obrey Chirwa na Donald Ngoma, kuelekea mchezo wao unaokuja wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mchezo wao uliopita, KMC walitoa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mwadui FC, uliochezwa Uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Ali alisema, katika mchezo wao uliopita hawakufurahishwa na matokeo waliyoyapata, hivyo hasira zao zote watamalizia kwa Azam, licha ya kukiri mchezo huo utakuwa mgumu.

ìKuna changamoto nyingi ambazo zilikuwa zinatukwamisha kupata matokeo, lakini mwalimu ameona na kuzitafutia ufumbuzi, nadhani mchezo wetu unaokuja ni dhidi ya Azam, tutahakikisha tunakabiliana nao vizuri na kuondoka na pointi tatu,î alisema.

KMC wanashika nafasi ya 11 katika msimamo wa Ligi wakiwa na pointi 18 katika michezo 14 waliyokwisha kucheza mpaka sasa, ambapo beki huyo amesema wanajiandaa kutoa dozi kwa kila timu itakayowasogelea.

MKWARA

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.