MAUGO ATAMBA KUMTWANGA MRUSI K.O

Dimba - - Dimba - NA GLORY MLAY

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Mada Maugo, ametamba kumchapa mpinzani wake, Batal Chezhia raia wa Urusi kwa K.O, katika pambano litakalofanyika Desemba 12 mwaka huu, kwenye ukumbi wa Bupas Gym uliopo Moscow.

Pambano hilo lisilo la ubingwa litakuwa la raundi 10 katika uzani wa Super middle kg 76.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Maugo alisema amejiandaa vya kutosha kuhakikisha anamaliza pambano hilo mapema kwa kumpiga mpinzani wake kwa K.O.

“Mpinzani wangu si bondia wa kunitisha, mimi nishakutana na mabondia wengi nchi tofauti na nimewapiga, naomba Watanzania waniombee nirudi na ushindi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.