Vishale Moro ina hali mbaya aisee!

Dimba - - Dimba -

CHAMA cha Vishale mkoani Morogoro (MOMDA), kimekiri kuporomoka kwa mchezo huo kutokana na kukabiliwa na ukata uliopiga kambi kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa Katibu wa Chama hicho, Bakili Anga, hali hiyo imesababisha timu za mkoa huo kushindwa kushiriki mashindano mbalimbali ya kitaifa.

Alisema mchezo hauna ufadhili wowote mkoani humo hali ambayo imewawia vigumu kushiriki mashindano mbalimbali.

"Hatuna ufadhili ndio maana tunashindwa kushiriki mashindano ya kitaifa, kinachofanyika wachezaji wetu ambao wamekuwa wakileta makombe wamekuwa wakicheza ndondo katika timu za mikoa mingine," alibainisha.

NA NYEMO MALECELA, MOROGORO

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.