Samatta kutoka Mbagala hadi Ubelgiji kama ndoto-3

Dimba - - Dimba - SIMULIZI NA SAADA SALIM

0676 010165 Ilipoishia TOLEO LILILOPITA NILIRUDISHA kumbukumbu ya utoto nikakumbuka jinsi alivyonitegemea na kuwa mmoja wa walezi wake wa karibu, nikakumbuka hata siku moja tulisahaulika kwenye basi wakati tukitoka Mbeya kuja Dar tukapishana na wazazi na tukaja Dar, kwa kweli niliumia sana siku hiyo nikaamua kufunga safari kwenda kambini kwao kumtazama, lakini kuendelea kumpa moyo ili aendelee kuichezea timu yake hiyo. Nikafika hadi kambini kwao nakumbuka ilikuwa Bamba Beach Kigamboni, nikamkuta yupo na wachezaji wenzake ambao wanalingana umri, aliponiona alionyesha tabasamu akiashiriia kwamba ana furaha kubwa katika moyo wake kwani ni kama nilienda kumtoa upweke. SASA ENDELEA .....

ULIKUWA msimu wake wa kwanza kuichezea Simba 2010/11, nilifika kambini Mbamba Beach mapema, aliponiona alifurahi sana, alionyesha kutamani kuniona.

"Kaka bora umekuja bwana hapa sio sahihi kwa mimi kuendelea kucheza hapa, najikuta mpweke kwa kweli sina amani," alisema lakini haya niliyatarajia.

Nilitumia muda mwingi kumshawishi abadili mawazo, nikaisifu Simba kwamba ni klabu kubwa na kwake ni bahati.

Nikampa mifano mingi ya wachezaji wenye ndoto ya kucheza timu kubwa kama hiyo lakini hawaipati.

Lakini nikamwambia kwa siri kwamba hapa Simba angeweza kupewa kitu chochote cha thamani hata ikiwemo gari, ilimradi tu afanye vizuri na viongozi wakubali kazi yake.

Sikuwa na shaka juu ya uwezo wake, lakini tatizo lile la kuwa mbali na mimi na hasa familia ndiyo lililokuwa jambo kubwa la kumshawishi.

Kilichonipa moyo ni kauli yake kwamba alikuwa akiishi vizuri na wenzake, hakukuwa hata na mchezaji mmoja ambaye wamewahi kukwaruzana hapo kambini hata kwenye mazoezi, hii ikanipa moyo.

Ukweli licha ya kumkubalia awepo Simba, lakini kila unapofika usiku nilikuwa namuwaza yeye endapo atalala salama au atakutana na changamoto zozote zile.

Nilikaa pale kambini kwa saa mbili hivi wakati najiandaa kurudi nyumbani nilimuahidi kwamba nitajitahidi kumpigia simu mara kwa mara, ikiwemo muda wa kumuamsha kwa ajili ya maandalizi ya kwenda mazoezi na muda anapokuwa anajisikia upweke. “Alinielewa na kufurahi baada ya hapo tuliagana na kwenda zangu nyumbani, nakumbuka wiki inayofuata tulikuwa tunakutana na Simba, hiyo ilikuwa mechi yake ya kwanza ya ligi lakini sisi wenyewe tuliita 'Dabi' iliyotukutanisha sisi ndugu wawili. Nilipofika nyumbani baba yetu mzee Samatta akaniweka chini akitaka nimweleze kiundani jinsi nilivyokutana na mwanawe (Samatta) na pia maisha anayoishi kule kambini. Muda mfupi baada ya kumaliza kutoa majibu yake kwa mzee, Samatta akanipigia simu akitaka kujua kama nimefika salama, sauti yake ilisikika yenye furaha. Baada ya kuzungumza na mzee nilitakiwa usiku kwenda kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Simba, baada ya kufika na kutulia chumbani kwangu dogo alinipigia simu kutaka kujua kama nimefika salama. Kumbe alikuwa na ujumbe mwingine kwangu.."Unajua mechi ijayo tunacheza na nyinyi African Lyon je, mmejipanga? akanitania. Sikufikiria nikatoa jibu la haraka tu, "Ndiyo ninajua na siku hiyo tutawafunga (Simba) mabao na kama huamini siku hiyo. wara huo akaujibu kimzaha akisema hayo mabao unayosema mtatufunga sisi sha yawe ndiyo nyinyi na hilo nitapachika nyewe kwa mguu Siku ya mechi alinipigia simu asubuhi na kurudia swali lake kwanza akauliza "mko fiti", baadaye akasema narudia tena leo tutawafunga mabao 2-0 na moja nitafunga mimi na kisha nitakuja kukuomba msamaha."

Matokeo yake yalikuwa hivyo hivyo Simba walitufunga mabao 2-0 na kweli bao moja alifunga yeye, nakumbuka alilia machozi na alinifuata kuniomba radhi.

Uzuri wake baada ya mechi hiyo timu zote zilivunja kambi, hivyo mimi na yeye tulirudi wote nyumbani na usiku ilikuwa kazi kubwa ya kubishana yeye akiwasilimua ndugu zetu kwamba hatuko fiti ndiyo maana wametufunga.

Tulipomaliza mechi tuliondoka wote nyumbani kwani sote tulivunja kambi, baada ya kufika nyumbani kula chakula na kupumzika alianza kunizodoa hatuko fiti kwani wangekuwa makini wangetupiga zaidi ya walizotufunga.

Usiku ule tuliongea mengi huku alinipa pongezi kwa siku ile niliyomshawishi hadi akakubali kubaki Simba, kwani alianza kuzoea maisha pale Msimbazi.

Nami nilimsifu pia kwa kuwa na misimamo yake ambayo hadi hii leo anaendelea, nakumbuka wakati fulani alipoahidiwa gari pale Simba ili asajili nilidhani anaweka mipango mizuri ya kupata usafiri wa kuwahi mazoezini.

Lakini kumbe ilikuwa ni msimamo wake tu, kwani hata alipokabidhiwa hilo gari bado aliliacha nyumbani, lakini kwa vile dhamira yake ilishatimia basi alikuwa akitoka usiku nyumbani na kuwahi mazoezi wakati huo yakifanyika katika Uwanja wa Uhuru (Shamba la bibi).

Kuna kipindi nilipata taairifa kwa wenzake kwamba, Mbwana anawahi sana mazoezi kiasi cha kufika uwanjani wakati giza likiwa bado limetanda na hivyo kulazimika kulala kwenye viti akisubiri wenzake.

Nilisikitika kusikia hivyo, nikaongea naye na kumpangia ratiba vizuri lakini kamwe hakubadili haraka msimamo wake wa kuwahi na nilipokuwa nikimuuliza kulikoni alisema anahitaji uvumilivu na kuzoea maisha yote huenda baadaye atafaidika. Simba ilimtengea kiasi gani na ilikiuwaje akatua TP Mazembe? Usikose Dimba Jumapili.

2-0 utaona Mkbu naye "Sasa hebu badilitutakayowafunga moja kati ya mimi mwewangu."

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.