Juma Abdul anahitaji somo jipya la unahodha

Dimba - - Dimba -

NA EZEKIEL TENDWA

JUMA Abdul ambaye ni nahodha msaidizi wa Yanga ambao ni mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara, anahitaji darasa maalumu ili akamilike vizuri kama kiongozi wa wachezaji wenzake hasa kutoka kwa Shadrack Nsajigwa.

Machi 2012 tulishuhudia vurugu kali katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, baadhi ya wachezaji wa Yanga wakimpa kipondo mwamuzi Israel Nkongo, kwa kutokuridhishwa na maamuzi yake mchezo dhidi ya Azam FC uliomalizika kwa Wanajangwani hao kulala kwa mabao 3-1.

Hata hivyo, aliyeibuka shujaa na kumwagiwa sifa kemkem alikuwa nahodha wa Yanga wa wakati huo, Shadrack Nsajigwa, kutokana na namna alivyokuwa akiwadhibiti wachezaji wenzake wasiendeleze vurugu.

Nsajigwa kama nahodha na kiongozi wa wenzake sio kwamba naye alikuwa hakerwi na maamuzi ya Nkongo katika mchezo huo, ila alisimama kama kiongozi kuhakikisha wachezaji wenzake hawakumbani na adhabu ambayo ingegharimu timu kwa ujumla.

Nimekumbuka kisa hicho baasan da ya Jumatatu ya wiki hii kushuhudia vurugu na hata kurushiana makonde na kupigana vichwa kwa baadhi ya wachezaji wa Yanga na wale wa Tanzania Prisons mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.

Vurugu hizo zilisababishwa na mchezaji mkongwe, Mrisho Ngassa, ambaye kwa makusudi kabisa aliamua kumtwanga kichwa HasKilichonishangaza Kapatala na hapo baadhi ya wachezaji wa Prisons uvumilivu uliwashinda wakajibu mapigo.

Ngassa alipewa kadi nyekundu kutokana na kitendo hicho lakini pia nahodha wa Prisons, Laurian Mpalile, naye alikumbana na adhabu hiyo baada ya kumpiga Ngassa kwa kichwa kutokana na hasira baada ya mwenzake kupigwa.

ni kutokana na Juma Abdul kushindwa kuwazuia wenzake katika vurugu hizo na badala yake yeye ndiye wa kwanza kwenda kurusha maneno kwa mwamuzi.

Juma Abdul alijisahau sana kwamba yeye ni kiongozi. Alishindwa kujitofautisha na akina Maka Edward, Ramadhan Kabwili, Rafael Daud na wengine ambao ni makinda ndani ya timu hiyo.

Nilimshangaa sana pia Mpalile, kwani yeye kama nahodha hakutakiwa kulipiza kwa kumpiga Ngassa kichwa na badala yake alitakiwa kuchukua jukumu la kwenda kulalamika kwa mwamuzi na pia kuamulia wenzake wasiwe na hasira.

Majukumu yote ya Juma Abdul katika purukushani zile yalichukuliwa na kijana mdogo, Feisal Salim ‘Fei toto’, ambaye ndiye aliyekuwa akiwasihi wenzake kuacha kubishana na maamuzi ya mwamuzi kwani ndiye aliyeshika mpini.

Katika tukio la kwanza la dakika ya 43, wachezaji wa Yanga wakionekana kugomea penalti iliyotolewa na mwamuzi, Fei ndiye aliyekuwa mstari wa mbele kuwaamua wasimzonge mwamuzi kwani alishatoa maamuzi.

Lilipokuja suala la Ngassa kumtwanga kichwa mwenzake, Fei pia ndiye aliyekuwa akiwasihi wenzake kutokuwa na jazba huku Juma Abdul ambaye ni nahodha na kiongozi akiwa mstari wa mbele kwenye kashkash hizo.

Katika kikosi kile cha Yanga kilichocheza kwenye mchezo huo, ukimuacha Ngassa, Juma Abdul ndiye mchezaji aliyecheza muda mrefu na anaijua Yanga ndani nje hivyo hata kama asingekuwa amevaa kitambaa cha unahodha, alitakiwa kuwa mstaarabu.

Juma Abdul anatakiwa kujifunza kwamba yeye ni kiongozi na mara kadhaa manahodha wenzake wanawaepusha wenzao na kadi zisizokuwa za lazima kwa kuwatuliza na jazba pale wanapoona mambo hayaendi kama wanavyotaka.

Pia hata Mpalile naye anatakiwa kujitathmini kwani yeye kama nahodha na kiongozi wa wenzake, hakutakiwa kuwa wa kwanza kwenda kushambulia wachezaji wa timu pinzani na badala yake alitakiwa kuwatuliza anaowaongoza.

Kwa kweli Juma Abdul na Mpalile wameniangusha sana, lakini lazima hapa nimpe sifa stahiki Fei Toto kwa kitendo cha kuvaa majukumu makubwa yaliyomzidi umri ya kupambana wenzake wasitishe vurumai.

Ni dhahiri Juma Abdul na Mpalile wanatakiwa kupata darasa maalumu na nini maana ya kuwa nahodha. Natamani darasa hilo walipate kutoka kwa Shadrack Nsajigwa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.