Mbao FC washusha vifaa vitatu matata

Dimba - - Dimba -

NA CLARA ALPHONCE MBAO FC wamechangamkia kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo baada ya kufanikiwa kunasa saini za wachezaji watatu kwa ajili ya kuboresha kikosi chao kuhakikisha wanatoa dozi kwa timu zitakazowasogelea.

Wachezaji hao wapya waliosajiliwa na kikosi hicho cha Mbao FC ni Gelvas Rambi kutoka African Lyon, Mekacha Mnata kipa kutoka kwa wanalambalamba Azam FC pamoja na Erick Mliko ambaye ni mchezaji huru.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Kocha Mkuu wa Mbao FC, Amri Said, alisema usajili huo ni mapendekezo yake na ameamua kufanya hivyo ili kuongeza kasi ya kikosi chake huku mawindo ya kusaka wachezaji wengine yakiendelea.

ìSasa hivi naangalia zaidi nafasi ya ushambuliaji, kwani kama unajua nchi yetu ina shida sana ya mastraika, lakini natamani sana kama ningempata mchezaji kariba ya Jerryson Tegete wa Kagera Sugar, angenisaidia sana, nimeshamwambia Kocha Mecky Mexime akitaka kumuacha anipe tu mimi, kwani namuhitaji sana,î alisema.

Alisema lengo lake ni kuiona timu hiyo ikimaliza moja ya nafasi za juu, ndiyo maana hata usajili wake unazingatia uwezo na nidhamu huku akikiri ipo idadi kubwa ya wachezaji walitamani kusajiliwa na kikosi hicho, lakini nafasi inabana.

USAJILI

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.