JKT Queens mambo safi WPL

Dimba - - Dimba - NA GLORY MLAY

KOCHA Mkuu wa mabingwa watetezi JKT Queens, Ally Ally, amesema kikosi hicho kipo fiti kutetea ubingwa wake katika Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara (WPL), inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Ally alisema wamefanya mazoezi ya kutosha na anaamini wachezaji wake watafanya vyema katika ligi hiyo ili kutetea taji lao.

Alisema hawana wasiwasi na klabu za Simba wala Yanga kwani wao wameimarika zaidi hivyo watakapokutana na timu hizo watachukua pointi tatu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.