Wavu ufukweni wasaka mil.8/-

Dimba - - Dimba - NA GLORY MLAY

MWENYEKITI wa Kamisheni ya Wavu Ufukweni Chama cha mpira wa Wavu Tanzania (TAVA), Shukuru Ally, amesema wanahitaji Sh mil.8 ili kufanikisha mashindano ya ‘Beach Volleyball’, yanayotarajiwa kuanza Desemba 8 mwaka huu, Coco Beach.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Ally alisema wanahitaji wadau kujitokeza kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kushirikisha timu 20 kutoka nchi mbalimbali.

Mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha timu 20 kutoka nchi mbalimbali ikiwamo Msumbiji, Burundi, Zanzibar, Rwanda, Kenya, Uganda na wenyeji Tanzania.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.