KHADIJA KOPA AVISHUKIA VYOMBO VYA HABARI

Dimba - - Dimba - NA JESSCA NANGAWE

M ALKIA wa taarabu nchini, Khadija Kopa, ametaja sababu ya muziki huo kushuka kwa kiasi kikubwa kumechangiwa na vyombo vya habari kuupa kisogo na badala yake kujikita kwenye muziki wa kizazi kipya.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Kopa alisema mbali na vyombo vya habari pia wasanii wenyewe wa muziki huo wameususa na kukata tamaa zaidi.

“Zamani muziki wa taarabu na dansi ndio ulikuwa unafanya vizuri lakini tangu Bongo Fleva waanze kuja juu, tumesahaulika sana na wao kujikita kwenye muziki wa kisasa, naamini kabisa tukipewa nafasi kama wenzetu tunarudi kwenye nafasi yetu,” alisema Kopa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.