AY: SIWEZI KUIPOSTI FAMILIA YANGU MTANDAONI

Dimba - - Dimba - NA JESSCA NANGAWE

N YOTA wa Bongo Fleva, Ambwene Yesaya, amesema moja ya sababu kubwa ya kutoposti picha ya mwanawe na mke wake kwa sasa ni makubaliano kati yao wawili.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, AY alisema haoni sababu ya kufanya hivyo katika mitandao ya kijamii kwa kuwa mwenye jukumu kubwa la kujua familia yake ni yeye peke yake na si watu wengine.

“Maisha ya kuposti vitu mitandaoni yakikuingia kichwani ni tatizo sana, ndo ile ikifika wakati humposti wanaanza kuulizana wameachana au, sioni sababu ya kuonyesha kila kitu kwenye maisha yangu, haya ni makubaliano yetu sisi,” alisema AY.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.