Si kila anayefanya kosa amekusudia

Dimba - - Dimba -

S IFA nyingi ziende kwa Mungu wetu aliyeumba ardhi na mbingu ambaye ameweza kutuwezesha kuikuta Jumatano ya kwanza katika mwezi Desemba ambao ni wa mwisho kwenye mwaka 2018.

Kama ilivyo kawaida ya kila Jumatano, tunakuwa pamoja katika safu pendwa ya Filamu za Kibongo zenye lengo la kutoa burudani na kutuelimisha mambo mbalimbali ya maisha ya kila siku.

Siku ya leo tunaiangalia filamu ya Uwoga inayowakutanisha wasanii mbalimbali wakiwemo Rehema Ally ‘Rihama’, Hashim Kambi ‘Mzee Kambi’ Mohamed Fungafunga ‘Mzee Jengua’ Abadallah Hamisi ‘Dulla’, David Justine na wengine wengi.

Filamu hiyo inaanza kwa kumwonyesha Munira ambaye ni mdogo wa Riyama akikimbizwa na watu waliotumwa na baba yake mdogo ‘Mzee Kambi’. Katika kutaka kujinasua anaingia kwenye chumba cha Dulla ambayo kilikuwa wazi.

Akiwa chumbani humo anatafuta sehemu ya kujificha, lakini mara anaingia Dulla na kushangaa kumwona binti akilia ndani kwake na anapojaribu kumuuliza anapewa majibu kuwa wanataka kumuua.

Dulla anakwenda kumuomba ushauri jirani yake ambaye naye anamtaka akatoe taarifa kwa mjumbe wa nyumba 10, lakini kwa bahati mbaya anaambiwa amesafiri lakini anamueleza mke wa mjumbe juu ya kile kilichomkuta kwa pamoja wanashauriana wamuache alale usiku huo na asubuhi ndio aondoke.

Dulla anakubaliana na ushauri huo lakini kwa bahati mbaya anapoamka asubuhi anamkuta Munira amefariki na hivyo anaingiwa na hali ya uoga kiasi cha kuchukua maamuzi ya kuuweka mwili wa Munira katika gunia kisha kwenda kumzika.

Baada ya siku mbili anaonekana Jengua akigombana na Kambi akimtaka arejeshe fedha zake alizompa kwani binti ambaye alipanga kumuoa (Munira) anatoroka.

Kambi anamuahidi kumtafuta Munira na anamlazimisha akubali kuolewa na ndipo Kambi anapompa taarifa Riyama juu ya kupotea kwa mdogo wake pamoja na harakati za kumtafuta zinavyoendelea. Riyama anasikitishwa na taarifa za mdogo wake amekimbia nyumbani baada ya kuwepo kwa suala la kulazimishwa kuolewa kwani kitu hiko ndicho kilichomkimbiza pia yeye kwa mjomba wake. Katika hangaika ya kumtafuta Munira, Riyama anakumbuka kuwa Dulla aliwahi kumwambia kuna msichana amekimbilia ndani kwake na hivyo kuwaeleza polisi juu ya jambo hilo na ndipo Dulla anapokamatwa kisha kukiri kufanya jambo hilo. Dulla anawapeleka polisi mahali alipoufukia mwili wa Munira na wanapoupeleka hospitali wanagudua Munira alifariki kwa presha na wala hakuuliwa kama ilivyokuwa ikidhaniwa na mwisho Dulla anaachwa huru.

...lakini kwa bahati mbaya anaambiwa amesafiri lakini anamueleza mke wa mjumbe juu ya kile kilichomkuta kwa pamoja wanashauriana wamuache alale usiku huo na asubuhi ndio aondoke.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.