TIMU YA USHINDI HAIBADILISHWI HOVYO AISEE!!

Dimba - - Dimba -

UNAKUMBUKA kikosi cha kwanza cha Simba kilichovaana na Mbabane Swallows mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kilikuwa ni hicho hicho jana katika mchezo wa marudiano. Katika mchezo wa marudiano uliochezwa Uwanja wa Mavuzo, nchini Eswatini zamani Swaziland, kipa alikuwa ni yule yule, Aishi Manula, mabeki Nicolaus Gyan, Mohamed Hussein, Erasto Nyoni na Pascal Wawa. Viungo: Jonas Mkude, James Kotei, Clataous Chama, huku washambuliaji wakiwa ni John Bocco, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi, huku Hassan Dilunga na Shiza Kichuya waliokuwa mwiba mchungu kwa wapinzani wakitokea benchi waliendelea kusubiria hapo hapo benchi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.