Torreira mkata shombo wa Arsenal

Dimba - - Dimba - NA ABDULAH MKEYENGE

KILA timu barani Ulaya ina kiungo wake anayekuwa matata katikati mwa uwanja. Na majukumu ya kiungo huyo yanakuwa ni kuiunganisha timu katika kukaba na kushambulia.

Muda mrefu Arsenal ilikosa mtu wa namna hii katika safu yake ya kiungo tangu majembe yake Patrick Vieira na Gilberto Silva walivyoondoka kikosini humo, lakini msimu huu wamempata mtu sahihi katika wakati sahihi. Ni Lucas Torreira anayefanya kazi ngumu katika kiungo cha Arsenal na kurahisisha kazi za nyota wengine kutamba.

Torreira amekuwa mtu wa shoka kweli. Hapishi mtu. Yeye ni kukata umeme kwa kwenda mbele. Jinsi jamaa anavyocheza mashabiki wa Arsenal wamembatiza jina la Ng’olo Kante mweupe wakimfafanisha na kiungo nyota wa Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.