Mechi mpya, tiketi za zamani

Dimba - - Dimba - NA ABDULAH MKEYENGE

HUKO Mbeya unaambiwa si mchezo. Juzi Jumatatu tulishuhudia mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Tanzania Prisons ‘Wajelajela’ dhidi ya Yanga na mashabiki wakiingia uwanjani kwa tiketi za msimu uliopita.

Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine ulishuhudia tiketi za vishina zikiwa na jina la mdhamini aliyemaliza muda wake, huku aibu kubwa ikiwa ni tiketi hiyo kuandikwa kwa msimu 2017/018 wakati huu ni msimu wa 2018/019.

Hilo ni moja ya tatizo sugu linaloonekana kukosewa tiba, lakini uingiaji madarakani wa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Ligi (TPLB), Steven Mguto, inaweza kuwa nafuu juu ya matatizo hayo ya mara kwa mara.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.