NI VITA YA KARNE

Dimba - - Dimba - ukichaa wa soka basi jaribu kutazama pambano hili. ya

NA NIHZRATH NTANI JNR J UMAPILI ya Desemba 9, 2018 kama uhai ungalipo na panapo uzima wa afya, Watanzania watakuwa wakisherehekea kimya kimya miaka 57 ya uhuru wa kujitawala kutoka kwa Mwingereza.

Ni usiku wa Jumapili hiyo hiyo ya Desemba 9, mamilioni ya mashabiki wa soka duniani kote, macho yao yataelekezwa kunako dimba la Santiago Bernabeu nchini Hispania. Ni kitu gani hicho kinaenda kutokea?

Hadithi ya timu mbili kutoka katika mji mmoja zinazotofautiana umbali wa kilomita 10 tu, wanapokutana nje ya Taifa lao, nje kabisa la bara lao. Inashangaza!!

Bila shaka umewahi kushuhudia au hata kusoma simulizi za timu mbili zenye uhasama na upinzani mkubwa katika soka?

Umewahi kusikia uhasama kati ya Atletico Madrid dhidi ya Real Madrid wanapokutana. Pengine umepata kuona pambano kati ya As Roma dhidi ya As Lazio.

Unapojaribu kusoma zaidi unapata kuona uhasama kati ya Everton na Liverpool, sahau kuhusu Tottenham na Arsenal ama Inter Milan na Ac Milan. Kote huko utakuwa unacheza tu. Unabakia kutabasamu peke yako.

Sote ni mashahidi, tumewahi kusikia na kuona uhasama uliopitiliza kati ya wababe wa mji mmoja au wapinzani katika soka. Tumepata kusikia vita ya Athen's kule Ugiriki. Wanapokutana Panathanakos na Olympiacos huwa ni vurugu isiyoelezeka.

Tunaweza kulitaja pambano kati ya Rangers dhidi ya Celtic kama vita ya itikadi ya kidini. Sahau kuhusu vurugu na kasheshe pale wanapokutana wahuni wa mji wa Istanbul kule Uturuki. Ni pambano kati ya Galatasaray dhidi ya Fenrbahce.

Wanapokutana Real Madrid dhidi ya Fc Barcelona, pambano lao linaitwa "EL Clasico". Vita hii huamuliwa ndani ya dakika 90 tu baada ya hapo kila mmoja hurudi katika majonzi na furaha yake.

Hili ndilo pambano maarufu zaidi duniani na lenye kutazamwa na mashabiki wengi baada ya fainali ya Kombe la Dunia.

Umewahi kusikia pambano lililobatizwa jina na kuitwa "Vita ya milele?" Ni pambano kati ya Partizan Belgrade na Red Star Belgrade. Hii ni zaidi ya soka.

Mashabiki kufa si jambo la kushtusha hata kidogo. Unapofikia hapo unabakia kujiuliza ni lipi pambano gumu zaidi kati ya hayo yote? Jibu hakuna, isipokuwa ... SUPER EL CLASICO

Ni umbali wa kilomita kumi, Kaskazini mwa mji wa La Boca ndani ya jiji la Buenos Aires, ndipo ilipo klabu ya Boca Juniors. Ni umbali huo huo ilipo klabu ya Boca Juniors unaporudi upande wa Kusini mwa mji wa La Boca unaipata klabu nyingine ya River Plate.

Hivi ndizo klabu mbili kubwa kabisa nchini Argentina. Wargentina wengi wanaamini kuwa zinapokutana klabu hizi mbili ndipo wanapokamilisha maana sahihi ya soka. Pambano la klabu hizi mbili linatajwa ndio baba wa "derby" duniani.

Pambano baina ya watu hawa, linachukuliwa kuwa ni pambano la karne, ni vita ya furaha na uhai. Ni pambano hatari zaidi kulitazama ndani ya uwanja, iwe La Bombonera unaomilikiwa na Boca Juniors ama kule Monumental de Nunez kwa River Plate.

Wakati fulani jarida mojawapo nchini Uingereza, lilipata kulitaja pambano kati ya miamba hii kama ni tukio la kipekee ambalo linakupasa ulitazame kabla hujaondoka duniani.

Nchini Argentina, soka ni sehemu ya imani na dini. Kufa kwa ajili ya kuipambania timu yako si kitu cha ajabu. Bila shaka kama unataka kuona NI VITA YA ADIDASNA NIKE

Kama ilivyo El Clasico kwa Nike kuidhamini Barcelona na Adidas kuikamata Real Madrid. Makampuni haya mawili yameendelea kupambana ndani ya "Super EL Clasico" kupitia timu hizi mbili. River Plate wakiwa chini ya Adidas wakati wapinzani wao wakiwa chini ya Nike.

Uwepo wa makampuni haya mawili ya vifaa vya michezo unaongeza msisimko fulani kwenye mawazo ya mashabiki wa soka. MWISHO WA UBISHI

Wakati mashabiki wa soka wakibakia kuwa na ndoto ya kushuhudia siku moja kuona El Clasico katika fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Bara la Amerika Kusini wamefanikisha hilo.

Novemba 11, 2018 ndani ya La Bombonera ndoto ikatimia kwa miamba hiyo miwili kukutana katika fainali ya Copa Libertadores. Michuano ambayo ina hadhi sawa na Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Pambano la Jumapili hii limepangwa kufanyika ndani ya dimba la Santiago Bernabeu nchini Hispania. Kilomita 10,039 sawa na maili 6,226. Ni mwendo wa saa 13 angani kutoka ndani ya jiji la Buenos Aires nchini Argentina hadi Madrid nchini Hispania.

Pambano la kwanza mwenyeji alikuwa Boca Juniors na matokeo yalikuwa sare ya 2-2 huku mechi ya marudiano ilipaswa kuchezwa Novemba 24 ndani ya Uwanja wa River Plate ila ilishindikana kutokana na matukio ya vurugu kwa mashabiki wa River Plate baada ya kuwashambulia na kuwajeruhi wachezaji wa Boca Juniors kwa mawe wakiwa ndani ya basi.

Pambano hili limeweza kuwateka mashabiki wengi wa soka duniani na miongoni mwao wamekuwa na shauku ya kulitazama pambano hili likifanyika kwa mara ya kwanza barani Ulaya. NANI ANAPEWA NAFASI KUBWA KUSHINDA?

Chini kocha Guillermo Barras Schelosto, Boca Juniors wanapewa nafasi kubwa kushinda dhidi ya kikosi cha kocha Marcelo Gallardo. Uwepo wa wachezaji; Carlos Tevez, Fernando Gago, Dario Benedetto, ndani ya kikosi cha Boca Juniors ni jambo la kujivunia.

Huku River Plate wakijivunia uhodari wa kipa wao Franco Armani, mshambuliaji wao Gonzalo "Pitty" Martinez na kiungo Juan Quintero. Pia tutawaona magwiji wa klabu hizi akiwemo Diego Maradona, Juan Roman Riqulme, Pablo Aimar, Gabriel Batistuta na wengineo wakiwa jukwaani.

Hata hivyo, klabu ya River Plate wanaendelea kupinga pambano hilo kupelekwa nchini humo. Tuendelee kusubiri kabla ya kushuhudia vita hiyo ya karne katika soka.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.