Tazara FC yaishushia kipigo Asante Africa

Dimba - - Dimba - NA NYEMO MALECELA, MOROGORO

T IMU ya soka ya Tazara FC imeishushia kichapo cha mabao 3-0 Asante Africa katika mechi ya Ligi Daraja la Nne kituo cha Ifakara, mkoani Morogoro.

Tazara ilianza kuonyesha ubabe wake kwa Asante Africa kipindi cha pili cha mchezo baada ya Yassin Mpanga kufanikiwa kufunga bao dakika ya 58, kabla Wisman Gabliely kupachika la pili dakika 68.

Jitihada za Tazara kutaka kusawazisha mabao hayo zilijikuta zikigonga mwamba kwa Mpanga kupachika bao la tatu dakika ya 77.

Msimamizi wa kituo hicho, Denis Kalomo, ameliambia DIMBA Jumatano kuwa mchezo huo ulikuwa na burudani za kipekee kutokana na upinzani wa timu hizo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.