Geita, Ambassador Simiyu zasonga mbele FA Cup

Dimba - - Dimba - NA DAMIAN MASYENENE, MWANZA

TIMU ya Geita Electric ya mkoani Geita imefanikiwa kusonga mbele katika hatua inayofuata ya michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC), baada ya kuichapa kwa mikwaju ya penalti 5-4 Munanira FC.

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Shule ya Wasichana ya Nyankumbu mjini Geita, Geita Electric walichomoza na ushindi huo ambapo sasa watakutana na mabingwa wa Mkoa wa Mwanza msimu uliopita, Phantom FC, Desemba 9, mwaka huu kwenye Uwanja wa Nyamagana.

Katika mchezo mwingine uliopigwa juzi mjini Tabora, wenyeji Majimaji FC walitupwa nje ya michuano hiyo baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 4-3 na Ambassador FC ya mkoani Simiyu baada ya dakika 90 za mchezo huo kushindwa kufungana.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.