Biashara United waichimba mkwara Yanga

Dimba - - Dimba - NA SHOMARI BINDAMUSOMA

TIMU ya Biashara United imetamba kujipanga kutibua rekodi ya kutokufungwa kwa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu uliopangwa kupigwa Desemba 9, mwaka huu Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, kocha msaidizi wa timu hiyo, Omary Madenge, alisema wanakwenda kuvaana na Yanga wakiamini sasa kikosi chao kiko fiti kuangusha mbuyu.

Alisema amezungumza na wachezaji baada ya mchezo dhidi ya Lipuli waliopoteza kwa kufungwa mabao 2-1 kwamba wanakwenda kukutana na timu ambayo inachagizwa na kufanya vizuri kwenye ligi, hivyo ni muhimu kujipanga namna ya kukabiliana nao.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.