Mkamba Rangers hawataki kusajili

Dimba - - Dimba - NA NYEMO MALECELA, MOROGORO

V INARA wa soka Ligi Daraja la Pili, Mkamba Rangers ya mkoani Morogoro, wamesema hawana mpango wa kufanya usajili dirisha dogo kwa kuwa kikosi kilichopo kina uwezo wa kupanda daraja.

Timu hiyo yenye pointi 11 tayari imeingia kambini jana kujiandaa na mechi mbili zilizobakia katika ngwe ya kwanza.

Kocha wa timu hiyo, Nicholas Makata, ameliambia DIMBA kuwa hana mpango wa kufanya usajili dirisha dogo bali anaongeza mazoezi kwa kikosi kilichopo ili kiweze kufanya vema kwenye mechi zilizosalia.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.