Ambokile awakataa Okwi, Kagere, Makambo

Dimba - - Dimba -

U NA JESSCA NANGAWE KISIKIA Uzalendo ndio huu unaoonyeshwa na straika wa Mbeya City, Eliud Ambokile, ambaye amesema kama yeye hatafanikiwa kuibuka mfungaji bora, basi angetamani atakayefanya hivyo awe mchezaji mzawa.

Ambokile ndiye anayeongoza kwa ufungaji akiwa amefikisha idadi ya mabao 9 akifuatiwa kwa ukaribu na Medie Kagere, Emmanuel Okwi (Simba), Heritier Makambo (Yanga)pamoja na Said Dilunga wa Ruvu Shooting kila mmoja akiwa na mabao saba.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Ambokile alisema, licha ya ushindani mkubwa unaoendelea wa kusaka ufungaji bora, anaamini huenda bahati hiyo ikamwangukia lakini akikosa yeye achukue mzawa.

"Kila mmoja anatamani kuwa mfungaji bora, ni bidii ya mtu tu, ukiangalia msimu uliopita ilikwenda kwa Okwi, sio kwamba wazawa hatuwezi , ni kujipanga na kuweka jitihada katika kufikia hilo.

"Ukweli natamani msimu huu mfungaji bora awe mchezaji mzawa, naamini hilo linawezekana kabisa kutokana na ubora

Aliongeza kuwa anategemea kuwepo na ushindani mkubwa wa nafasi hiyo hasa upinzani unaoletwa na wachezaji wa kimataifa lakini lengo lake ni kujipanga kikamilifu na kuhakikisha anajitengenezea nafasi nzuri zaidi.

Ukiachilia Ambokile, ushindani wa nafasi hiyo upo kwa wachezaji watatu wa kimataifa Okwi, Kagere pamoja na Makambo sambamba na mchezji wa Ruvu Shooting Said Dilunga ambao wote wamefungana kwa mabao saba kila mmoja.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.