MODRIC: NA BADO MTANUNA SANA

Dimba - - Dimba - MADRID, HISPANIA

M SHINDI wa tuzo ya Ballon d’Or, Luka Modric, amewashangaa ambao walisema hakustahili kushinda tuzo hiyo kuwa wana wivu juu ya mafanikio yake.

Modric anakuwa mchezaji wa kwanza baada ya miaka 10 ya utawala wa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ambao walitwaa tuzo hiyo mara tano kila mmoja.

“Nafikiri wanaona wivu au wanaumizwa na mafanikio yangu, nashukuru wachezaji wenzangu kwa kuniunga mkono,” alisema Modric.

Kiungo huyo raia wa Croatia aliisaidia timu yake ya taifa kutinga fainali ya Kombe la Dunia ambayo walifungwa mabao 4-1 na Ufaransa, lakini pia alikuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa Real Madrid waliotwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.