Lukaku atupia tena Man United ikipeta FA

LUKAKU ATUPIA TENA MAN U IKIPETA FA

Dimba - - Mbele -

R OMELU Lukaka kwa mchezo wake wa tatu mfululizo na kuisaidia Manchester United kutinga raundi ya nne Kombe la FA baada ya jana kuwafunga Reading mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Old Tra΍ord.

Reading ambao inacheza katika Ligi Daraja la Kwanza walianza vizuri lakini alikuwa ni Juan Mata aliyewapatia Manchester United bao la kuongoza kwa mkwaju wa penalti kabla ua Lukaka kuongeza bao la pili kupindi cha pili.

Huu ulikuwa ni ushindi wa tano mfululizo kwa tangu Manchester United wampatie kazi Ole Gunnar Solskjaer.

Kocha huo wa muda katika mchezo wa jana, alibadilisha kikosi chake kiasi na kuwapa nafasi baadhi ya wachezaji chipukizi akiwemo kipenzi cha mashabiki, Andreas Pereira.

Tangu Solskjaer akae kwenye benchi la ufundi la United akisaidiana na Michael Carrick, timu yao hiyo iliibuka na ushindi kwenye michezo minne mfululizo, huku ikiwa imefunga mabao 14 kwenye mechi hizo.

Hata hivyo, timu ambazo Solskjaer aliwaongoza vijana wake kuzisaka pointi tatu muhimu zilikuwa ni Cardi΍, Huddersȴeld, Bournemouth na Newcastle.

Timu hizo nne zote zipo ndani ya nafasi tano za chini kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, ikiwa na maana kwamba Solskjaer alikutana na ratiba nzuri ya kuanzia maisha mapya ya ukocha Old Tra΍ord.

Lakini hiyo haiwazuii mashabiki wa Man Utd kufurahia matokeo ya mechi zao za hivi karibuni tangu klabu yao hiyo ilipoamua kumtimua Jose Mourinho.

Ujio wa Solskjaer kwenye kikosi cha United umeamsha morali kwa kiasi kikubwa na kuchangia timu hiyo kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-1, 3-1, 4-1 na 2-0 katika mechi hizo nne.

Baada ya kutengeneza kikosi kazi kwa ajili ya kuokoa heshima ya Man Utd ambayo inashikilia nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, Solskjaer, atawaongoza nyota wake kuchuana na Tottenham.

Mechi hiyo itakayochezwa Januari 13, wikiendi ijayo, ndilo jaribio gumu zaidi kwa Man Utd tangu Solskjaer awe kocha wa timu hiyo.

Wakati Man Utd ikishikilia nafasi ya sita na pointi zao 38, sita pungufu ya Chelsea ambao wapo kwenye nafasi ya nne, Tottenham wao wanajitanua katika nafasi ya tatu wakiiacha United kwa tofauti ya pointi 10.

Hata hivyo, kwa kutazama kiwango bora cha Man Utd kwa sasa, ni wao ambao wanaonekana kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuibuka na ushindi kwenye mtanange huo.

United ndiyo timu pekee mpaka sasa ambayo haijapoteza mchezo tangu kuanza kwa kipindi cha sikukuu, mwishoni mwa Desemba mwaka jana, lakini Tottenham nao hawapo mbali sana.

Wakali hao wa London wanaifuatia United baada ya kushinda mechi zao tatu na kupokea kichapo kimoja kwenye Ligi Kuu England.

Wakati Red Devils wakiringia uwepo wa washambuliaji hatari, Marcus Rashford, Anthony Martial na Romelu Lukaku, wakisaidiwa na kiungo, Paul Pogba ambaye kiwango chake kimeimarika mno tangu Mourinho aondoke, Spurs nao wana silaha za hatari.

Harry Kane, Christian Eriksen, Dele Alli na Lucas Moura, ni nyota waliosaidia Spurs kufanya vyema katika siku za hivi karibuni.

Wanaozifuata timu hizo ni Liverpool na Leicester (nazo zikiwa zimeshinda mechi nne na kupoteza moja).

Crystal Palace (5), Arsenal (6), Chelsea (7) na Manchester City (8), nazo zipo kwenye kiwango bora mno ndani ya wiki moja tangu kuanza kwa kipindi cha sikukuu.

Zilizofanya hivyo ni Everton, Newcastle, Huddersȴeld ambayo imepoteza mechi zote nne.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.