Mwambao Bonanza kurindima leo

Dimba - - News - NA HENRY PAUL

BONANZA la soka linaloshirikisha timu za maveterani wa Ukanda wa Mwambao, linatarajiwa kufanyika leo kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mikocheni jijini Dar es Salaam kuanzia saa 2:00 asubuhi na kumalizika saa 12:00 jioni.

Akizungumza na DIMBA, Mwenyekiti wa Bonanza hilo, Lusozi Faza, alizitaja timu zitakazoshiriki katika bonanza hilo kuwa ni Bagamoyo Veteran, Boko Veteran, Mbezi Beach Veteran, Mwenge Veteran, Wazee wa Kazi Veteran, Mbweni Veteran, GMK Veteran na wenyeji Mikocheni Veteran.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.