KUMBE HARMONIZE HANA MPANGO WA KUOA

Dimba - - Burudani - NA JESSCA NANGAWE

MSANII wa Bongo Fleva kutoka lebo ya WCB, Rajab Abdul maarufu kama Harmonize, amesema licha ya kushauriwa na mama yake kuhusu kuoa lakini kwa sasa bado hana mpango huo.

Harmonize ambaye kwa sasa yupo kwenye mahusiano na mwanadada, Sarah raia wa Italia, pia alishawahi kutoka na staa wa Bongo Movie, Jackline Wolper, kabla ya wawili hao kubwagana.

Akizungumza na DIMBA, Harmonize, alisema anafahamu umuhimu wa maisha ya ndoa lakini kwa sasa jambo hilo bado halijawa kwenye akili yake.

"Nafurahi kuona wasanii wa Bongo Fleva wameamka na sasa wengi wanaoa, ni jambo zuri lakini kwangu naona muda bado..labda 2025 huko ndio naweza kuwaza mambo hayo," alisema Harmonize.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.