Tena Dah! P. Diddy avurugwa

Dimba - - Burudani -

HUKU akiwa bado ana maumivu ya kuondokewa na aliyewahi kuwa mama watoto wake, rapa mkongwe, P. Diddy, amekumbwa na majanga mengine.

Kim alishaachana na Diddy muda mrefu lakini mwanamke huyo aliyemzalia watoto wanne anaaminika kuwa alikuwa akipendwa mno na staa huyo.

Sasa wakati Diddy akiendelea kuuguza kidonda, mpenzi wake wa miezi michache iliyopita, Cassie Ventura (32), ameamua kumtibua.

Diddy (45) alianza kutoka kimapenzi na Cassie tangu mwaka 2007 lakini kila mmoja alichukua ‘50’ zake Oktoba, mwaka jana. Alichoamua kukifanya Ventura ni kuposti picha inayomwonesha akiwa na mpenzi wake mpya, Alex Fine, lengo likiwa ni kumuumiza Diddy.

Katika kile alichodai ni makusudi, mmoja kati ya watu wa karibu wa msanii huyo alisema: “… hakukuwa na haja ya kuposti picha hiyo kipindi hiki. Diddy ana wakati mgumu kwa sasa.”

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.