MABEKI, VIUNGO WAPIGWA ‘BAO LA KISIGINO’ NA MASTRAIKA TPL

Dimba - - Dimba Special -

WACHEZAJI wanaocheza nafasi ya ulinzi sambamba na wale wanaohudumu eneo la kiungo ‘wamefunikiwa’ na washambuliaji kwa ujumla Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo iko tamati mzunguko wa kwanza kwa timu kadhaa. Hatua hiyo inatokana na tuzo za mchezaji bora wa mwezi kuchukuliwa na wachana nyavu pekee tangu Agosti hadi Desemba mwaka jana tofuti kabisa na msimu uliopita. Tuzo hizo ambazo mshindi anaambulia shilingi milioni moja, Agosti ilienda kwa Meddie Kagere wa Simba akifuatiwa na Eliud Ambokile wa Mbeya City (Septemba), Emmanuel Okwi (Simba, Oktoba) na Heritier Makambo (Yanga, Novemba na Desemba).

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.