PLUIJIM 'ANUNUA' UGOMVI WA YANGA

Dimba - - Mbele - NA TIMA SIKILO, ZANZIBAR

UKISIKIA kununua ugomvi basi ndilo huku, kwani baada ya Yanga kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Malindi katika michuano ya Mapinduzi, Kocha Mkuu wa Azam FC, Hans Van der Pluijm, amesema wabaya hao wa kikosi chake hicho cha zamani watapata tabu sana leo.

Yanga walijikuta wakitupwa nje ya michuano hiyo baada ya kukubali kichapo hicho cha mabao 2-1 na leo wanakamilisha tu ratiba watakapocheza dhidi ya Jamhuri, huku Azam wakicheza dhidi ya Malindi.

Azam na Malindi zimeshafuzu hatua ya nusu fainali, huku Yanga na Jamhuri wakitupwa nje kutokana na kupata matokeo mabaya kwenye michezo yao iliyopita, hivyo leo zinakamilisha ratiba na kufungasha kila kilicho chao.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Pluijm alisema hawataki kupoteza mchezo wowote kwenye michuano hiyo, kwani lengo lao ni kutetea ubingwa wao.

“Utakuwa mchezo mgumu, lakini sisi tumejiandaa kuhakikisha tunashinda, kwani tumekuja na lengo moja tu la kutetea ubingwa wetu, najua upinzani ni mkubwa, lakini tutafanikiwa,” alisema.

Akimzungumzia straika wake, Yahya Zayd, ambaye amekwenda kukipiga Ismailia ya Misri, alisema kinda huyo ni mmoja wa wachezaji wanaojituma sana na kwamba atapata mafanikio makubwa zaidi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.