Straika wa Malindi alitaka kukutana na Yondani

Dimba - - News - NA TIMA SIKILO

STRAIKA wa Malindi ya Zanzibar ambayo imeitupa Yanga nje ya michuano ya Mapinduzi, Juma Balana Prince, amesema alitamani kukutana na kikosi kamili cha Wanajangwani hao chini ya safu ya ulinzi ya Kelvin Yondani, ili wawaonyeshe kazi.

Malindi wamewatupa Yanga nje ya michuano hiyo baada ya kuwafunga mabao 2-1 na leo wanacheza dhidi ya Jamhuri ya Pemba kukamilisha ratiba.

Akizungumza na DIMBA jana, Balana, ambaye alifunga bao la pili na la ushindi, alisema moja ya ndoto zake ilikuwa ni kuifunga Yanga, japo wachezaji aliokuwa ametarajia kupambana nao hawakuja Zanzibar.

Balana alifanikiwa kuifunga Yanga katika mchezo wa juzi kipindi cha pili, ambapo bao la kwanza la timu yao liliingizwa kimiani na Abdulswamadu Kassim Ali.

“Ninafurahi kwamba tumewafunga Yanga, hilo ni jambo ambalo nilikuwa nalisubiri sana, japo nasikitika kwamba wachezaji wao wa kikosi cha kwanza hawakuja.

“Furaha yangu ingekuwa kubwa zaidi kama tungewafunga wakiwa kamili kama Kelvin Yondani, Ibrahim Ajib, Makambo (Heritier) na wengine, lakini ndiyo hivyo tena hawakufika.

“Unajua Mapinduzi kwetu ni sawa na kombe la dunia, tunaithamini sana hii michuano na ndiyo maana tukifanikiwa kuzifunga timu kubwa kama Simba, Yanga na Azam, mambo yanakuwa ni mazuri sana,” alisema.

Katika hatua nyingine, strai-

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.