Daba wawaangukia wadau

Dimba - - News - NA ZAINAB IDDY

MWENYEKITI wa Chama cha Ngumi za Ridhaa Mkoa wa Dar es Salaam (DABA), Godfrey Akolory, amewaomba wadau wa mchezo huo kuwasaidia vifaa pamoja na zawadi za washindi kwa ajili ya mashindano mbalimbali mwaka huu.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Akolory alisema mwaka uliopita walikuwa na uhaba mkubwa wa vifaa, jambo lililosababisha mara kwa mara washindwe kuandaa mashindano kwa wakati.

ìMwaka 2018 haukuwa mzuri kwa Daba, kwani mara kwa mara tulilazimika kuahirisha mashindano kutokana na kukosa vifaa vya michezo, ikiwemo glovu, lakini pia hata zawadi za washindi hatukuwa nazo.”

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.