Gigy Money adai yeye ni mke bora

Dimba - - Burudani - NA JESSCA NANGAWE

MSANII wa Bongo Fleva, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money, amesema licha ya watu wengi kuamini yeye ni mtu wa kupenda starehe, lakini hawajui kuwa yeye ni mke na mama bora wa familia. Gigy Money ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwaye Mayra, amesema kuna watu wamekuwa wakimhukumu kuwa hajui malezi na pia amekuwa mtu wa starehe zaidi lakini mwenyewe amekanusha na kusisitiza akiwekwa ndani yeye ni mke bora. “Kuna watu wamekuwa wakinihukumu kwa mambo mengi, wengine wanadiriki kusema hata sijui kumlea mwanangu, lakini hawajui kwa sababu mimi nikiwekwa ndani, huwezi kudhani ni Gigy ambaye wamezoea kuniona kwenye matamasha ya muziki akinengua viuno,” alisema Gigy Money.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.