Penzi linaweza kuondoa furaha ya familia

Dimba - - Burudani - NA ZAINAB IDDY

KARIBU msomaji wa safu ya simulizi za Filamu za Kibongo inayokujia kila Jumatano katika gazeti lako la Dimba Jumatano, leo tunaiangalia sehemu ya pili ya kazi inayoitwa Nyumba ya uasherati.

Katika filamu hii wapo wasanii mbalimbali wakiwemo, Chuchu Hansi, Herry Samir ‘Mr Blue’, Elizabeth Michael ‘Lulu’ Kajala Masanya, Seleman Barafu, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Wema Sepetu na Libert Msuya. Ilipoishia.. Libert anakimbilia kijijini kwao kuanza maisha mapya huko nako anakutana na janga la kumpa binti mwingine mimba lakini wakati akitafakari rafiki yake anampigia simu na kumwambia arudi mjini baada ya hali kutulia lakini pia anampa dili lingine.

Libert anarejea mjini na kwenda kufanya kazi nyumbani kwa Barafu huko anakutana na Wema (mke wa Barafu), Kajala (dada wa Barafu), Lulu (mtoto) na binti wa kazi ambayo wote wanaonyesha kumkubali kutokana na utendaji kazi wake.

Tuendelee..

Kadiri siku zinavyokwenda familia hiyo inaonekana kuingiwa na pepo wa uasherati baada ya wote hao kuonyesha nia ya kumhitaji Libert kimapenzi kipindi ambacho baba mwenye mji Barafu akiwa safarini.

Bila kujua nini madhara ya kile kinachofanyika, Libert anaamua kuwapanga mmoja mmoja familia nzima akianza na mama mwenye nyumba (Wema), mtoto (Lulu), Shangazi (Kajala) na dada wa kazi kwa kuwapa mapenzi moto moto kiasi cha kujikuta kila mmoja akimhitaji muda wote.

Kitendo cha kila mmoja katika familia ya Barafu kumhitaji Libert kinazua ugomvi baina yao unaosababisha kutokuwa na maelewano mazuri kitu kinachoonekana kumkera Libert ambaye anaona wazi siku si nyingi kibarua chake kitaota nyasi.

Libert anajaribu kuongea na wanawake zake kila mmoja kwa nyakati tofauti akiwataka wapunguze wivu na kumnyima uhuru wa kuwa karibu na wengine kwani unaweza kuhatarisha kazi yake. Baada ya miezi mitano kupita akiwa katika penzi moto moto na wanawake waliokuwa kwenye familia ya Barafu, siku moja baba mwenye nyumba anarejea na kukuta ugomvi kati ya mdogo wake Kajala na binti yake Lulu. Katika kuwahoji nini wanagombania lakini anakosa jibu la maana kwa wawili hao jambo linalomchanganya kwani mazingira aliyoyakuta katika familia yake hayamridhishi. Siku moja anawaita watu wote waliokuwa nyumbani kwake kuwaambia nataka kufanya sherehe kidogo ya kumshukuru Mungu kwa kumrejesha nyumbani salama kila mmoja anafurahishwa na jambo hilo. Siku ya sherehe inafika wakiwa pamoja wanakula na kunywa mara Lulu anainuka na kwenda kutapika wakati akitafakari hili Kajala naye anafuata huku nyuma mkewe Wema akitoka mbio kwenda bafuni kabla ya msichana wao wa kazi kukutwa na tatizo hilo hilo.

Kitendo cha kutapika familia nzima hasa wanawake kinamchanganya na kuamua jukumu la kuwapeleka hospitali wote na ndipo inapogundulika wote ni wajawazito.

Barafu anafurahishwa juu ya ujauzito wa mkewe Wema lakini anapata mashaka kuona dada yake, mwanawe na msichana wa kazi wote wana mimba na hivyo kuwaweka kitimoto kutaka awatajie nani aliyefanya uchafuzi huo.

Baada ya Barafu kuwabana sana familia yake, ukweli unajulikana kuwa aliyefanya hivyo ni Libert kitu kinachompandisha hasira na kuamua kwenda kuchukua panga ili ampige.

Kabla ya kufanya tukio la kumpiga Libert mara anaingia Shilole akiwa na kaka yake na kuhoji nani aliyempa mimba mdogo wake na ndipo Libert anapotajwa kwa mara nyingine na wote kujikuta wakishangaa.

Kitendo cha kutapika familia nzima hasa wanawake kinamchanganya na kuamua jukumu la kuwapeleka hospitali wote na ndipo inapogundulika wote ni wajawazito.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.