TBF kuanzisha ndondo kikapu

Dimba - - Sultan - NA GLORY MLAY

RAIS wa Shirikisho la mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa, amesema wana mpango wa kuanzisha mashindano ya ndondo ya kikapu ili kuzidi kukuza mchezo huo hapa nchini.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Magesa alisema mashindano hayo yatasaidia pia kuendelea kukuza vipaji vya vijana waliopo mitaani.

Alisema kwa kufanya hivyo anaamini kikapu kitazidi kukua na wachezaji chipukizi wengi watapatikana ambapo vipaji vyao vitaendelezwa kwa ajili ya mashindano hapo baadaye kwa namna moja au nyingine.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.