agombea Yanga watema cheche

Dimba - - Mbele - NA MWANDISHI WETU

IKIWA ndiyo siku ya kwanza kuzinduliwa kwa kampeni za uchaguzi katika klabu ya Yanga, baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali wamezungumza na DIMBA Jumatano na kuweka bayana mikakati yao.

Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti katika uchaguzi huo, Baraka Igangula pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Athanas Kazige, ambao walizindua kampeni zao Temeke Kata ya 15 jijini Dar es Salaam, wamesema hii ndiyo nafasi adimu ya kuinusuru Yanga, iliyofika mikononi mwao.

Igangula alisema uongozi wa klabu hiyo kongwe ulipoteza mwelekeo ambao sasa unahitaji watu sahihi kwa ajili ya kuirudisha taasisi hiyo katika mstari.

Aliwapongeza wana Yanga na hasa kocha Mwinyi Zahera pamoja na wachezaji ambao wamekuwa wakijituma katika kipindi ambacho klabu imekosa mwelekeo kutokana na kukosa uongozi stahili ambao yeye na kamati yake wanakuja kurudisha heshima iliyokuwepo.

Kwa upande wake Kazige, ambaye ni mwandishi mkongwe wa habari za michezo na pia mchambuzi wa vipindi vya michezo Redio Uhuru, alisema ameamua kujitosa kugombea nafasi hiyo ili kutumia taaluma yake kuiwezesha klabu yake kongwe kupiga hatua.

Wajumbe wengine waliokuwepo katika uzinduzi huo ni pamoja na Said Ramadhani na Mwakasonda Haule.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.