TFF watoa neno uchaguzi Yanga

Dimba - - News - NA SALMA MPELI

KUELEKEA uchaguzi wa Yanga, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Malangwe Mchungahela pamoja na Mjumbe wa Kamati ya utendaji wa Yanga, Siza Lyimo, wamewataka wagombea wote kwa kushirikiana na wanachama wa klabu hiyo kufanya kampeni za utulivu na amani.

Hayo yamezungumzwa jana katika kikao cha pamoja na Wanahabari kilichofanyika katika ukumbi wa TFF Karume, ambako jana ndiyo ilikuwa siku rasmi ya uzinduzi kwa kampeni hizo.

Kwa upande wake Siza, aliwataka Wanayanga kulipia kadi zao mapema, ili kupata nafasi ya kushiriki katika uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Januari 13 mwaka huu, kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Osterbay.

“Tunaomba wanachama na wagombea waliojitokea ili kujaza nafasi zilizo wazi kwenye uchaguzi huo, kampeni ziwe na utulivu na amani, kusiwepo na kashfa wala kunyoosheana vidole, pia uchaguzi utakuwa wa uhuru, haki na utulivu, wanachama wajitokeze kwa wingi,” alisema Siza.

Kwa upande wake Mchungahela, alisema amefungua rasmi zoezi la kampeni na kuwataka wanachama kushirikiana vizuri na wagombea hao, wasikilize sera zao ili Januari 13 wajue wanaokwenda kuwachagua.

“Wanachama wote wenye kadi za Yanga wataruhusiwa kupiga kura, iwe kadi zile za zamani za kitabu na zile kadi za benki ambazo zimehakikiwa, wote ni wanachama halali na wana haki ya kupiga kura,” alisema Mchungahela.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.