Evergreen yaigeukia Simba Queens

Dimba - - News - NA GLORY MLAY

KOCHA wa Evergreen, Omary Nyango, amesema baada ya kuchapwa mabao 9-0 na JKT Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Bara, sasa hasira zote anazihamishia kwenye mchezo wao na Simba Queens.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam ambapo Evergreen watakuwa wenyeji.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Nyango alisema, wamejipanga kuhakikisha wanachukua pointi tatu ili kujiweka katika mazingira ya kutokushuka daraja msimu huu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.