Timu za Vishale zaitwa Tada Cup

Dimba - - News - NA GLORY MLAY

KLABU za vishale nchini zimetakiwa kujitokeza kwa wingi kuthibitisha ushiriki wao kwenye mashindano ya Tada Cup, yatakayofanyika Machi mwaka huu, Tabora.

Mashindano hayo yatasaidia kupatikana kwa wachezaji watakaounda kikosi cha timu ya taifa, kitakachoiwakilisha nchi kwenye mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Vishale Tanzania (Tada), Subira Waziri, alisema kuwa maandalizi ya awali ya michuano hiyo yanaendelea vizuri.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.