OBFT ruksa kupewa ofisi Uwanja wa Taifa

Dimba - - News - NA ZAINAB IDDY

BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limebariki Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (OBFT) kupewa ofisi katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, kama watahitaji.

Tangu kufanyika kwa uchaguzi wa OBFT na kuapishwa kwa viongozi wake, chama hicho kimeshindwa kuwa na ofisi yao, ambalo BMT imesema kila chama kilichopo chini yake lazima kiwe na ofisi ya kufanyia kazi, hii ni kwa mujibu wa sheria.

Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Alex Nkenyenge, alisema kama OBFT wamekosa sehemu ya kuweka ofisi zao wafuate taratibu za kupata chumba Uwanja wa Taifa na waachane na mpango wa kufanyia kazi mifukoni.

PICHA NA JOHN DANDE

Mchezaji wa Simba B, Juma Abdalah (kushoto), akimtoka Salum Mkeyenge, katika mazoezi yaliofanyika Uwanja wa Kinesi, Dar es Salaam jana.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.